Faragha na ulinzi wa taarifa

Sera ya Faragha

Taarifa tunazokusanya

Tunakusanya taarifa unazowasilisha kwa hiari kupitia ombi la huduma, oda ya kitabu, supplier application, stakeholder portal au WhatsApp baada ya WhatsApp Business API kuunganishwa. Hizi zinaweza kujumuisha jina, simu, barua pepe, shirika, anwani ya usafirishaji na maelezo ya ombi.

Matumizi ya taarifa

Taarifa hutumika kujibu ombi, kutekeleza oda, kuthibitisha malipo, kuwasiliana kuhusu huduma, kusimamia usalama na kuboresha huduma. Ziara za kawaida hupimwa kwa jumla bila kuunda wasifu binafsi wa mtumiaji.

WhatsApp na taarifa za afya

Ujumbe wa WhatsApp unaweza kurekodiwa kiotomatiki baada ya API kuunganishwa ili timu ifuatilie huduma. Usiwasilishe taarifa nyeti za kitabibu kupitia fomu ya kawaida; kwa dharura wasiliana na kituo cha afya kinachofaa.

Uhifadhi na usalama

Tunatumia access control, roles, activity logs, encryption ya usafirishaji na backups. Taarifa huhifadhiwa kwa muda unaohitajika kutekeleza madhumuni yake na wajibu halali wa biashara; muda mahususi wa retention utathibitishwa na menejimenti.

Haki na mawasiliano

Kwa ombi la kuona, kusahihisha au kufuta taarifa zinazokuhusu, wasiliana na info@shekemu.co au +255 714 147 181.